Pata taarifa kuu
IRAQ-SIASA

Iraq: Uchaguzi wa Urais waahirishwa tena kwa kukosa akidi inayohitajika kikanuni

Nchini Iraq, wabunge walitarajia kumchagua rais wa Jamhuri Jumamosi Machi 26, miezi sita baada ya uchaguzi wa wabunge. Lakini kikao kiliahirishwa kwa mara ya pili kutokana na kukosekana kwa akidi inayohitajika kikanuni.

Nchini Iraq, kwa mara ya pili, wabune hawakufikia akidi ya inayohitajika kikanuni kuendelea na uchaguzi wa rais wa Jamhuri.
Nchini Iraq, kwa mara ya pili, wabune hawakufikia akidi ya inayohitajika kikanuni kuendelea na uchaguzi wa rais wa Jamhuri. © AP/Hadi Mizban
Matangazo ya kibiashara

Jaribio jingine limeshindwa. Kwa mara ya pili ndani ya miezi sita, abunge hawakufikia akidi inayohitajika kikanuni ili kuendelea na uchaguzi wa rais wa Jamhuri. Wabunge 202 walikuwepo Jumamosi hii, lakini idadi ya wabunge 220 ilihitajika ili kura hiyo ifanyike. Sababu: wito wa kususia uliotolewa na vyama vilivyo na uhusiano wa karibu na Iran.

Tangu uchaguzi wa mwezi Oktoba, muungano huu umeondolewa kwenye mazungumzo kati ya pande zinazopingana kumchagua rais mpya na waziri mkuu. Muungano huu mwingine wa Kishia, unaoongozwa na Moqtada Sadr, mshindi mkubwa wa uchaguzi wa wabunge, unataka kulazimisha wagombea wake na kuunda kile kinachoitwa serikali ya wengi, ambapo vyama vinavyounga mkono Iran havitakuwa na wizara.

Mwenendo ambao unavunja mila ya Iraq, inayoheshimiwa tangu uchaguzi wa kwanza mwaka 2005, na ambayo inataka viongozi hawa wa kisiasa watoke kwenye maelewano kati ya makundi mawili makubwa ya Kishia. Kambi mbili kuu za kisiasa ambazo zinapingana leo, zaidi ya hapo awali.

Uchaguzi mpya umepangwa kufanyika Jumatano ijayo, kujaribu kumaliza mgogoro wa kisiasa, ambao umesababisha nchi hiyo inashindwa kupata serikali mpya kwa miezi sita sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.