Pata taarifa kuu

India yatuma tani 2,500 za ngano hadi Afghanistan katikati mwa mzozo wa kiuchumi

Nchini Afghanistan, raia wanaendelea kuteseka kutokana na mgogoro wa kibinadamu: fedha nyingi za umma za serikali zilizuiwa baada ya Taliban kuchukua mamlaka. Waafghan wanakosa kila kitu kuanzia dawa hadi chakula. Ili kuwasaidia, India imekutuma shehena ya tani 2,500 za ngano, kwa njia ya nchi kavu, kwa kutumia barabara za adui yake, Pakistani.

Msafara wa malori 50 yaliyokuwa na rangi za bendera ya India ndiyo umeingia Pakistani na tani 2,500 za ngano na kukabidhi Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, lililoko Jalalabad, Afghanistan.
Msafara wa malori 50 yaliyokuwa na rangi za bendera ya India ndiyo umeingia Pakistani na tani 2,500 za ngano na kukabidhi Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, lililoko Jalalabad, Afghanistan. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Msafara wa malori 50 yaliyokuwa na rangi za bendera ya India ndiyo umeingia tu Pakistani kuwasilisha tani 2,500 za ngano kwa shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, huko Jalalabad, Afghanistan.

Kwa mujibu wa balozi wa Afghanistan nchini India, Farid Mamundzay, ni mojawapo ya misaada mikubwa zaidi ya chakula kutoka kwa nchi hiyo tangu mgogoro wa kibinadamu uliosababishwa na vita na mamlaka kuchukuliwa na Taliban.

Malori kutoka India kwa kawaida hayaruhusiwi nchini Pakistan, lakini Islamabad iliidhinisha kwa hatua ya kipekee kwa msafara huu wa kibinadamu mwishoni mwa mwezi Novemba, wiki sita baada ya ombi la India.

Kwa takriban mwaka mmoja, India, ambayo ilikuwa na uhusiano wa karibu na serikali ya awali ya Afghanistan iliyoungwa mkono na nchi za Magharibi, pia imetoa dozi 500,000 za chanjo ya Covid-19 na tani 13 za dawa na nguo.

Afghanistan haina pesa yoyote ya akiba tangu Taliban kurejea madarakani na kusimamishwa ghafla kwa msaada wa kimataifa mwezi Agosti, ambao umekuwa ukifadhili karibu 80% ya bajeti ya Afghanistan, na vile vile Marekani kuzuia dola bilioni 9.5 katika Benki Kuu ya Afghanistan.

Afghanistan imetumbukia katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi unaotishia njaa kwa raia wake. Umoja wa Mataifa ulizungumzia juu ya hali "muhimu" ya kibinadamu na idadi kubwa ya wakaazi milioni 28 wanaohitaji msaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.