Pata taarifa kuu

Mpango wa nyuklia ya Iran: Rais Raïssi anyooshea kidole cha lawama Marekani na Ulaya

Katika mpango wa nyuklia ya Iran, mvutano unaendelea wakati mataifa makubwa yakiitaka Iran kurejea kwenye meza ya mazungumzo ya Vienna yakiwa na wasiwasi kuhusu maendeleo makubwa katika mpango wa nyuklia wa Tehran.

Rais wa Iran Ebrahim Raïssi akitembelea kiwanda cha nyuklia cha Bushehr Oktoba 8, 2021.
Rais wa Iran Ebrahim Raïssi akitembelea kiwanda cha nyuklia cha Bushehr Oktoba 8, 2021. via REUTERS - OFFICIAL PRESIDENTIAL WEBSITE
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Iran Ebrahim Raïssi amezitolewa wito nchi za Magharibi, akisema Ulaya na Marekani ndio wanatakiwa kufanya maamuzi ya kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya Vienna ambayo yamesitishwa kwa takriban miezi mitano.

Tehran inaiomba Washington kuondoa vikwazo vyote vilivyowekwa tangu mwaka 2018 na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ambaye aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya nyuklia.

Tatizo, "kukataa kuchukuwa maamuzi"

“Kinachotatiza Marekani na Ulaya ni kukataa kuchukuwa maamuzi. Hawachukui uamuzi. Tumefanya uamuzi wetu ambao ni kuheshimu makubaliano na tumeheshimu hilo. Tatizo linatokana na ukweli kwamba upande mwingine hauchukui uamuzi, "amesema Ebrahim Raïssi.

Kauli hii mpya inakuja wakati Iran imeongeza kasi ya mpango wake wa nyuklia kwa kuongeza kwa kiasi kikubwa hifadhi yake ya uranium iliyorutubishwa, ambayo inaendana na makubaliano ya 2015. Tehran pia inafanya 20% na 60% ya urutubishaji, zaidi ya kizingiti kilichoidhinishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.