Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Nyuklia: Iran kushiriki mazungumzo kwa minajili ya kuondolewa 'vikwazo vyote'

Tehran imetangaza kuwa mazungumzo na mataifa makubwa juu ya suala lake la nyuklia yataanza tena, lakini bila kutoa tarehe maalum. Rais mpya wa Iran Ebrahim Raïssi amechukua msimamo thabiti ambao unatia wasiwasi Marekani na nchi za Magharibi wakati Iran imeongeza kasi kwa shughuli zake za nyuklia.

Rais wa Iran Ebrahim Raïssi ahutubia hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya video, Septemba 21, 2021.
Rais wa Iran Ebrahim Raïssi ahutubia hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya video, Septemba 21, 2021. AP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mkuu mpya wa diplomasia, Tehran yuko katika harakati za kuunda timu mpya ya kuanza tena mazungumzo ya Vienna. Lakini imekataa mkutano wa mawaziri wa kundi la 4 + 1 huko New York, kama ilivyotaka Ufaransa, amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.

Kwa upande wake, rais wa Iran Ebrahim Raissi pia amekosoa vikali Marekani katika hotuba yake kwa nji ya video wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa: "Marekani haikuheshimu ahadi zake ambazo zilikuwa kufutwa kwa vikwazo. Ilijiondoa kwenye mkataba wa nyuklia na kuweka vikwazo vingi dhidi ya raia wangu. Hatuamini ahadi za serikali ya Marekani. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaona kuwa mazungumzo pekee ndio yatakayowezesha kufutwa kwa vikwazo. "

Kufutwa kwa vikwazo kabla ya mazungumzo

Majadiliano na Iran yamekwama tangu mwishoni mwa mwezi Juni. Timu mpya ya mazungumzo ya Iran itakuwa na msimamo mkali wakati mazungumzo yataanza tena.

Wakati huo huo mkuu mpya wa mpango wa nyuklia wa Tehran ametangaza kuwa Marekani lazima ifute vikwazo "kabla" ya kuanza tena kwa mazungumzo. Hapo tu, ameongeza, ndipo Iran itakubali tena kupunguza mpango wake wa nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.