Pata taarifa kuu
IRAN

Nyuklia: IAEA yafikia makubaliano na Iran juu kuendelea kukagua vituo vya nyuklia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia (AEA), ambaye mkuu wake Rafael Grossi yuko Tehran Jumapili, Septemba 12, limetangaza kwamba limefikia makubaliano na Iran juu ya suala la vifaa vya ukaguzi wa mpango wa nyuklia, siku kadhaa baada ya kukemea ukosefu wa ushirikiano kutoka Jamhuri ya Kiislamu.

Mkuu wa IAEA Rafael Grossi, ambaye yuko Tehran, alisema amefikia makubaliano na Iran siku ya Jumapili juu ya kuendelea kukagua vituo vya nyuklia.
Mkuu wa IAEA Rafael Grossi, ambaye yuko Tehran, alisema amefikia makubaliano na Iran siku ya Jumapili juu ya kuendelea kukagua vituo vya nyuklia. AFP - ALEX HALADA
Matangazo ya kibiashara

Iran inaonekana kupiga nusu hatua kuelekea IAEA, amebaini mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi. Mkuu mpya wa mpango wa nyuklia nchini humo Mohammad Eslami ametaja mazungumzo aliyofanya na Rafael Grossi kuwa yalikuwa mazuri. Ameongeza kuwa wataendelea na mazungumzo na kubaini kwamba mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa atarejea Tehran kwa mazungumzo zaidi.

Hata hivyo Iran itaendelea kuhodhi mikanda yote ya video inayorikodiwa kwenye vituo vyake vya nyuklia wakati mazungumzo ya kuzishawishi Jamhuri hiyo ya Kiislamu na Marekani kurejea kwenye mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 zikiwa zimeambulia patupu.

Kadhalika haijafahamika iwapo Iran itakabidhi mikanda ya video iliyorikodiwa miezi iliyopita ambayo serikali mjini Tehran ilikwishatishia kuiharibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.