Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Raissi: Tuko tayari kuanza tena mazungumzo, lakini hatutokubali kushinikizwa

Akihimizwa na nchi za Magharibi kuanza tena mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia na mataifa yenye nguvu duniani, rais wa Iran Ebrahim Raissi amesema Iran iko tayari kuanza tena mazungumzo, lakini sio kwa shinikizo na vikwazo.

Rais wa Iran Ebrahim Raissi alisema yuko tayari kuanza tena mazungumzo ya nyuklia na nchi za Magharibi "lakini sio kwa shinikizo".
Rais wa Iran Ebrahim Raissi alisema yuko tayari kuanza tena mazungumzo ya nyuklia na nchi za Magharibi "lakini sio kwa shinikizo". AFP - HO
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Iran, ambaye alizungumza kwenye runinga ya serikali, alikuwa wazi kabisa katika matamshi yake, akisema kwamba Iran haitaki mazungumzo kwa shinikizo.

Kwa kweli tuna mazungumzo na majadiliano juu ya ajenda ya serikali, lakini sio kwa shinikizo. Shinikizo hizi zinazoandamana na mazungumzo hazijatoa matokeo yoyote hapo awali, Marekani na mataifa ya Ulaya wanaamni hiki ninachoongea. Hatutarudi nyuma hata kidogo kwa masilahi ya wananchi wa Iran.

Katika siku za hivi karibuni, mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani na Urusi waliishinikiza Tehran kuanza tena mazungumzo huko Vienna ili kufufua makubaliano ya mwaka 2015 na kuwezesha kuondolewa kwa vikwazo vya Amerika dhidi ya Iran. Baada ya hayo, Iran itakubali kupunguza mpango wake wa nyuklia tena.

Lakini kwa sasa, hakuna tarehe iliyotolewa na Tehran. Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir Abdollahian hata hivyo alisema ilikuwa ni lazima kusubiri miezi miwili au mitatu kabla ya timu mpya ya washauri wa nyuklia kuanza kazi.

Kauli hii inatia wasiwasi sio tu mataifa ya Magharibi, bali pia Israeli, ambayo inakosoa maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika maswala ya nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.