Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Iran yadai kuwashikilia maafisa wanaofanya kazi kwa niaba ya Israeli

Vikosi vya usalama vya Iran vimewakamata kundi la watu wanaodaiwa kufanya kwa niaba ya Israeli na kugundua silaha kadhaa ambazo Tehran inasema zilikusudiwa kutumiwa katika maandamano dhidi ya uhaba wa maji ambayo yameikumba Jamhuri ya Kiislamu kwa wiki mbili, vyombo vya habari rvya serikali vimeripoti leo Jumanne.

Kulingana na afisa wa wizara ya ujasusi ya Iran aliyenukuliwa na vyombo vya habari vya serikali, bastola, mabomu, bunduki na risasi vimekamatwa na vikosi vya usalama vya Iran.
Kulingana na afisa wa wizara ya ujasusi ya Iran aliyenukuliwa na vyombo vya habari vya serikali, bastola, mabomu, bunduki na risasi vimekamatwa na vikosi vya usalama vya Iran. REUTERS/Lisi Niesner
Matangazo ya kibiashara

Tehran inashtumu maadui au wapinzani wake kama Israeli, Marekani na Saudi Arabia, kwa kujaribu kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuchochea maandamano na vurugu.

Iran inakabiliwa na ukame mbaya zaidi tangu miaka 50 iliyopita, na maandamano dhidi ya uhaba mkubwa wa maji, ambayo mwanzoni yaliripotiwa kusini-magharibi mwa nchi iliyoathiriwa hasa, yamechukua sura ya kisiasa na kuenea katika maeneo mengine katika siku za hivi karibuni.

Mamlaka inawashutumu wapinzani wenye silaha kwa kusababisha mapigano wakati wa maandamano, wakati mashirika ya haki za binadamu yakishtumu vikosi vya usalama kwamba viliwafyatulia risasi waandamanaji.

Kulingana na afisa wa wizara ya ujasusi ya Iran aliyenukuliwa na vyombo vya habari vya serikali, bastola, mabomu, bunduki na risasi vimekamatwa na vikosi vya usalama vya Iran.

"Maafisa wa Mossad (idara ya ujasusi ya Israel) walipanga kutumia silaha hizi wakati wa ghasia za mijini na kwa mauaji", ametangaza afisa huyu bila kutoa maelezo zaidi.

Viongozi wa Israeli hawajasema chochote juu ya madai hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.