Pata taarifa kuu
ISRAEL

COVID-19: Israeli yaanza kampeni ya chanjo

Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu amezindua rasmi kampeni ya chanjo dhidi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Waziri mkuu wa Israel, Benyamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel, Benyamin Netanyahu Menahem Kahana/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo linakuja wakati kunaripotiwa ongezeko la visa vya maambukizi wa virusi vya Corona wakati wengi wanafikiria kuhusu iwapo serikali huenda ikachukua kwa mara ya tatu masharti mapya dhidi ya Corona. Israel ambayo ina waakazi Milioni tisa imerekodi zaidi ya visa 370,000, pamoja na vifo 3,057.

 

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alikuwa wa kwanza nchini Israeli kupewa chanjo hiyo. Zoezi hilo lilirushwa moja kwa moja kwenye vituo vyote vya Televisheni wakati taarifa za habari za jioni. Kwa kutoa mfano mzuri, Benjamin Netanyahu alisema: "Tunaweza kusema: Mtu mmoja kudungwa sindano, anaokoa afya ya watu wote. Ninakutakieni mafaanikio mema. Nendeni mpewe chanjo. "

 

Kampeni ya chanjo inaanza leo Jumapili hii nchini Israeli. Kwanza, kwa kuwapa chanjo wafanyakazi wa afya. Wakifuatiwa na watu wenye umei wa zaidi ya miaka 60 na wale walio na magonjwa sugu.

 

Kinga ya pamoja inatarajiwa kutolewa mwezi Mei 2021

 

Kwa jumla, Israeli imeagiza zaidi ya dozi milioni 14 za chanjo kutoka kwa maabara ya Moderna na Pfizer. Wataalam wa afya wamebaini kwamba mwishoni mwa mwezi Mei kinga ya pamoja inaweza kupatikana nchini. Lakini wakati huo huo, idadi ya visa vipya imeongezeka.

 

Baraza la mawaziri linatarajiwa kuchukua hatua zaidi dhidi ya COVID-19 leo mchana, pamoja na kufunga biashara ambazo sio muhimu. Na kuanzia asubuhi ya Jumapili hii, watu wote wanaoingia Israeli watalazimika kuwekwa karantini kwa wiki mbili; hii pia ni pamoja na Waisraeli wanaorejea kutoka Falme za Kiarabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.