Pata taarifa kuu
ISRAELI-USALAMA-SIASA

Israeli yakumbwa na maandamano

Maelfu ya raia wa Israel, wakiwa wamevaa barakoa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, wameendelea kuandamana katika mji wa Tel Aviv dhidi ya waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Maandamano yanaruhusiwa nchini Israeli licha ya hatua zilizochukuliwa kukabiliana na janga la Covid-19, ambapo waandamanaji wanaheshimu sheria za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Maandamano yanaruhusiwa nchini Israeli licha ya hatua zilizochukuliwa kukabiliana na janga la Covid-19, ambapo waandamanaji wanaheshimu sheria za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Benjamin Netanyahu, Waziri anaye maliza muda wake anatarajiwa kuhukumiwa mwezi ujao wa Mei kuhusu madai ya ufisadi, ambayo ameendelea kukanusha.

Bw. Netanyahu anaendelea na mazungumzo na hasimu wake kutoka mrengo wa kati, Benny Gantz, kiongozi wa muungano wa chama cha mrengo wa kati, Blue and White alliance, kuhusu makubaliano ya muungano wa serikali ili kumaliza uhasama wa kisiasa unaodumu sasa mwaka mmoja, baada ya chaguzi tatu za wabunge ambazo walishindwa kupata idadi kubwa ya wajumbe katika Bunge la Israel (Knesset).

Maandamano yanaruhusiwa nchini Israeli licha ya hatua zilizochukuliwa kukabiliana na janga la Covid-19, ambapo waandamanaji wanaheshimu sheria za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Wakishikilia bendera nyeusi, waandamanaji hao walikuwa wakiimba katika maamnadamano yao ya Jumapili "Tuilinde demokrasia", huku wakitoa wito kwa Benny Gantz asifikie makubaliano na Waziri Mkuu anayeshutumiwa makosa ya ufisadi.

Gantz aliahidi wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba serikali ya baadaye itakuwa "safi" lakini tangu wakati huo, alisema kuwa mgogoro wa kiafya unamlazimisha atenguwe ahadi yake.

Zaidi ya visa 13,000 vya maambukizi na vifo 172 vinavyohusiana na ugonjwa huo vimeripotiwa nchini Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.