Pata taarifa kuu
MAREKANi-IRAQ-IRAN-USALAMA

Iraq: Marekani yafanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya wanamgambo wa Iran

Marekani imeendesha mfululizo wa mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya wanamgambo wa Iran ikijibu shambulizi la roketi lililogharimu maisha ya askari wawili wa Marekani na askari mmoja wa Uingereza katika kambi ya jeshi Kaskazini mwa Baghdad.

Wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Iraq, Hachd al-Chaabi, katika Mkoa wa  Anbar nchini Iraq Novemba 12, 2018 (picha ya kumbukumbu).
Wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Iraq, Hachd al-Chaabi, katika Mkoa wa Anbar nchini Iraq Novemba 12, 2018 (picha ya kumbukumbu). AHMAD AL-RUBAYE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapema mchana, Pentagon iliwanyoshea kidole cha lawama wanamgambo wanaounga mkono serikali ya Iran kwamba walihusika katika shambulio hilo dhidi ya kambi ya jeshi ya Taji, shambulio ambalo pia lilijeruhi watu 14.

"Marekani imefanya mashambulizi ya kujihami dhidi ya mitambo ya kundi la Kataib Hezbollah kote nchini," ilisema taarifa ya Pentagon na kuongeza kuwa mashambulizi hayo "ni jibu la moja kwa moja kwa tishio lilifanywa na wanamgambo wa Kishia wanaoungwa mkono na Iran".

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper, alinukuliwa katika taarifa hiyo, akiionya kwamba Marekani itachukua "hatua muhimu kulinda vikosi vyake nchini Iraqi na katika ukanda wa Mashariki ya Kati".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.