Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTURUKI-SYRIA-USALAMA

Marekani yakanusha madai ya kuwapa silaha Wakurdi

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex  Tillerson  amesema nchi yake haijawahi kuwapa silaha nzito wapigani wa Kikurdi nchini Syria.

Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, wakati wa ziara yake mjini Beirut Februari 15, 2018.
Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, wakati wa ziara yake mjini Beirut Februari 15, 2018. REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Tillerson imekuja wakati akiwa jijini Beirut nchini Lebanon, alipoulizwa kuhusu mchango wa Marekani kwa wapiganaji hao ambao Uturuki inasema ni magaidi.

Tillerson amezuru pia Uturuki, kujaribu kuimarisha uhusiano kati ya nchi yake na Syria kuhusu mapambano ya Ankara dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi.

Akiwa Beirut, Rex Tillerson alikanusha kwamba uhusiano kati ya Washington na Ankara uko matatani kwa sababu ya mashambulizi ya jeshi la Uturuki yanayoendelea kaskazini magharibi mwa Syria. Katika kanda hii, na zaidi hasa katika mji wa Afrin, vikosi vya Kikurdi ambavyo Washington inasaidia dhidi yakundi la Islamic State vinakabiliwa na mashambulizi ya jeshi la Kituruki.

Rais Erdogan aliishtumu Marekani kuwapa silaha wanamgambo wa Kikurdi wa YPG.

Hata hivyo Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Rex Tillerson amekanusha na kusema kuwa hawajawahi kuwapa silaha Wakurdi.

Rex Tillerson hivi karibuni alishtumu mashambulizi ya Uturuki dhidi ya ya ngome ya wapiganaji wa Kikurdi ya Afrin. Lakini Kwa mujibu wa Bw Tillerson, Uturuki bado ni "mshirika muhimu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.