Pata taarifa kuu
ISRAEL-USALAMA

Shimon Peres kuzikwa katika makaburi ya Mount Herzl

Shimon Peres atazikwa Ijumaa hii 3 Septemba 30 katika makaburi ya Mount Herzl mjini Jerusalem. Mahali kunakozikwa watu ambao walichangia kwa ujenzi wa nchi na mahali pa makumbusho kwa Waisrael wengi waliouawa katika mazingira tofauti.

Katika makaburi ya Mount Herzl, wafanyakazi wakichimba kaburi la Rais wa zamani wa Israel Shimon Peres.
Katika makaburi ya Mount Herzl, wafanyakazi wakichimba kaburi la Rais wa zamani wa Israel Shimon Peres. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa kigeni zaidi ya mia moja wanatarajiwa kuhuduria Ijumaa hii, Septemba 30, mazishi ya aliyekuwa Rais wa Israel na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Shimon Peres, mjini Jerusalem. Alifariki Jumatano akiwa na umri wa miaka 93kufuatia maradhi ya kiharusi.

Wajumbe 90 kutoka nchi 70, usalama kuimarishwa

Bendera zimepandishwa nusu mlingoti nchini kote Israel, polisi ikiendelea kuimarisha usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo,. Jumla ya wajumbe 90 kutoka nchi 70 wanatazamiwa kuhudhuria sherehe hizo.

Israel haijawahi kushuhudia tukio kama hilo tangu mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani Yitzhak Rabin mwaka 1995. Yitzhak Rabin, ambaye alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel pamoja na Shimon Peres na kiongozi wa Wapalestina Yasser Arafat mwaka 1994, aliuawa na Myahudi mwenye msimamo mkali.

Miongoni mwa viongozi wa dunia watakaokuepo Ijumaa katika mji wa Jerusalem ni pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama na mtangulizi wake Bill Clinton. Rais wa Ufaransa, François Hollande, pia ataongozana na mtangulizi wake Nicolas Sarkozy. Charles Prince au Mfalme wa Uhispania watahudhuria sherehe hizo za mazishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.