Pata taarifa kuu
ISRAEL-SHIMON PERES

Shimon Peres alazwa hospitalini

Rais wa zamani wa Israel na kiongozi aliyetunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel Shimon Peres, mwenye umri wa miaka 93, amelazwa hospitalini kwa dharura Jumanne usiku karibu na mji wa Tel Aviv na kupatishiwa msaada wa vifaa vya kumsaidia kupumua baada ya kupatwa na kiharusi, ofisi yake imearifu katika taarifa yake.

Rais wa zamani wa Israel na Shimon Peres, Novemba 14, 2015 mjini Tel Aviv.
Rais wa zamani wa Israel na Shimon Peres, Novemba 14, 2015 mjini Tel Aviv. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Rais wa zamani amelazwa katika hospitali ya Tel Hashomer kutokana na kiharusi."

Baada ya kusema kwamba hali yake ilikuwa "imara" na alikuwa na "fahamu" ofisi ya Bw Peres imearifu kuwa kumetokea "mabadiliko katika hali yake ya afya."

"Madaktari wake wameamua kumuweka dawa ya usingizi na kumpatishia vifaa vya kumsaidia kupumua ili kurahisisha namna ya kumuhudumia. Ndani ya dakika chache, alikua anatazamiwa kupitishwa katika chombo cha Scanner ili kutathmini zaidi hali yake ya afya," ofisi yake imesema.

Vyombo vya habari nchini Israel inaarifu kwamba Peres alikuwa katika hali mbaya.

Vyombo vya habari vimewatuma waandishi wao katika mji wa Ramat Gan karibu na mji wa Tel Aviv. Tel Hashomer ni hospitali kubwa nchini Israel.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amemtakia rais huyo wa zamani wa Israel kupona haraka. Shimon, tunakupenda na wananchi wote wana matumaini kuwa utapona," ameandika Netanyahu kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Netanyahu amekutana na mkurugenzi wa hospitali ili kujua kuhusu hali ya Peres, ofisi yake imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.