Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFGHANISTAN

Shambulizi dhidi ya Chuo Kikuu cha Marekani katika mji wa Kabul

Milio ya risasi na milipuko vimesikika Jumatano hii Agosti 24 katika Chuo Kikuu cha Marekani katika mji wa Kabul, nchini Afghanistan. Wanafunzi, ambapo baadhi yao walifungiwa ndani ya jengo la Chuo Kikuu hiki, wameshuhudia milipuko na milio ya risasi. Hadi sasa, hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusia na shambulio hili.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan katika eneo la shambulizi mjini Kabul Jumatano hii, Agosti 24.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan katika eneo la shambulizi mjini Kabul Jumatano hii, Agosti 24. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Chuo Kikuu cha Marekani katika mji wa Kabul kimelengwa Jumatato hii kwa shambulizi la watu wenye silaha. Washauri wa Kimarekani wa ujumbe Resolute Support wamesaidia polisi ya Afghanistan kukomesha shambulizi hili, kwa mujibu wa afisaa aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.

Hakuna kundi lililodai mpaka sasa kuhusika na shambulizi, ambalo linakuja wiki mbili baada ya walimu wawili wa chuo kikuu, mmoja kutoka Australia na mwengine raia wa Marekani kutekwa nyara.

Walimu hawa wawili walitekwa nyara na watu wenye silaha waliokuwa walivalia sare ya polisi jioni ya Agosti 8 katika mji wa Kabul, utekaji nyara huo ulilenga raia wa kigeni.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari anayejitegemea, Mustafa Kazemi, shambulizi limemalizika baada ya washambuliaji kuuawa, na kutangazwa na polisi. Wanafunzi kwa sasa wako salama na Massoud Hossaini, mpiga picha wa shirika la habari la Associated Press, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Pulitzer, aliyekuwa ameshikiliwa katika majengo ya Chuo Kikuu hicho wakati wa shambulizi, amejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.