Pata taarifa kuu
URUSI-SYRIA-USHIRIKIANO-USALAMA

Syria: Putin yuko tayari kupeleka askari wake Syria

Wakati ambapo ndege za Urusi zikiendelea kuondoka nchini Syria, rais wa Urusi ameonya kuwa jeshi lake linaweza, ikiwa itahitajika, kurudi kwa mara nyingine nchini humo "ndani ya masaa kadhaa".Vladimir Putin ameonya kwamba kama makundi ya waasi yatakiuka mkataba wa usitishwaji wa mapigano, Mosco haitosita kujibu.

Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wa Kremlin, Moscow, Machi 17 2016.
Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wa Kremlin, Moscow, Machi 17 2016. REUTERS/Alexei Nikolsky/Sputnik/Kremlin
Matangazo ya kibiashara

Urusi haijifichi,imejikubalisha kulinda eneo la anga la Syria, na kusaidia majeshi ya nchi kavu ya Syria. Ingawa hakukuwa na takwimu sahihi za wanajeshi wa Urusi nchini Syria, wataalamu wanakadiria 6000 idadi ya askari wa Urusi ambao walikuwepo nchini Syria. Idadi hii inaweza kupungua hadi 1000, wengi wao wakiwa washauri, mafundi na maafisa wa Idara ya Ujasusi, kwa kulisaidia jeshi la Syria.

Kuhusu ndege, wataalam wanakisia kuwa kati ya ndege 50 na 70 za Urusi zilitumwa nchini Syria, lakini ndege hizo zilikua zikibadilishwa mara kwa mara, na hivyo idadi hiyo kuwa ngumu kutambua. Mashambulizi ya anga zaidi ya 6,000 yalitekelezwa na ndege za Urusi kwa mujibu wa takwimu za serikali.

Putin bado anadhibiti kambi mbili za jeshi

Hata hivyo, ndege za msaada kwa wanajeshi wa nchi kavu zitabaki. Ni ndege ambazo si rahisi risasi kupenya, na zina uwezo wa kubeba mizigo mikubwa. wajibu wa ndege hizo ni kulinda askari wa Syria nchi kavu. Watasaidiwa katika kazi hii kwa helikopta aina ya MI 24 na 35.

Ili kuhakikisha udhibiti wa anga la Syria, Urusi ina ndege za kivita aina ya SU 30 na 35, zinazohusika na kukabiliana na ndege ya adui.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.