Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAEL-MAUAJI-USALAMA

Palestina: watu tisa wauawa Gaza, wawili Jerusalem

Vijana wawili wa Kipalestina wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa Jumamosi baada ya kufyatuliwa risasi na vikosi vya usalama vya Israel katika Ukanda wa Gaza, katika eneo la mpaka na Israel, Idara ya huduma dharura imebaini.

Wapalestina wakibeba mwili wa Ahmed Qali wakati wa mazishi yake katika kambi ya wakimbizi ya Chouafat katika Jerusalem ya Mashariki, Oktoba 10, 2015.
Wapalestina wakibeba mwili wa Ahmed Qali wakati wa mazishi yake katika kambi ya wakimbizi ya Chouafat katika Jerusalem ya Mashariki, Oktoba 10, 2015.
Matangazo ya kibiashara

Kifo cha Marwan Barbakh, mwenye umri wa miaka 13, na Khalil Othman, mwenye umri wa miaka 15, wakati wa mapigano mashariki mwa mji wa Khan Younis kimepelekea kufikia idadi ya vijana tisa wa Kipalestina ambao wameuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama vya Israel tangu Ijumaa katika eneo la mpaka na Israel katika ukanda wa Gaza.

Mapigano yalitokea tena Jumamosi hii katika maeneo mengi ya eneo la mpaka na Misri katika eneo la ukanda wa Gaza, wakati ambapo Wapalestina na Waisrael wamejihusisha tangu Oktoba 1 katika ongezeko la machafuko katika Ukingo wa Magharibi na Mashariki ya Jerusalem.

Wapalestina ishirini wameuawa, ikiwa ni pamoja na watu saba waliohusika na mashambulizi kwa visu na Waisrael 4 tangu Oktoba 1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.