Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-MAPIGANO-USALAMA

Syria: zaidi ya wakaazi 300 wa Palmyra wauawa na IS

Wakati ambapo Islamic State ikiendelea kuwatuma wapiganaji wake wapya katika mji wa Ramadi, magharibi mwa Iraq, nchini Syria, siku moja baada ya kiongozi wa Kishia wa Hesbollah kutoka Liban kutoa wito wa kuungana dhidi ya Islamic State, wito mwingine wa kuokoa mji huo wa kale wa Palmyra, umetolewa na viongozi wa Chuo kikuu cha Al-Azhar nchini Misri.

Mji wa kale wa Palmyra, tarehe 14 Machi mwaka 2014. Unesco imeomba Jumatano wiki hii, kusitishwa kwa mapigano ili kuokoa mji huo wa kihistoria.
Mji wa kale wa Palmyra, tarehe 14 Machi mwaka 2014. Unesco imeomba Jumatano wiki hii, kusitishwa kwa mapigano ili kuokoa mji huo wa kihistoria. AFP PHOTO / JOSEPH EID
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Palmyra uko chini ya udhibiti wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Kwa mujibu wa Shirika la haki za binadamu nchini Syria, wanamgambo wa kundi hilo waliendesha mauaji hivi karibuni katika mji wa Palmyra na vitongoji vyake.

Taarifa ya mauaji yaliyotekelezwa na wanamgambo wa Islamic State zimetolewa na vyanzo vya serikali vya Syria na upinzani. Picha za kwanza ziliyorushwa na kundi hilo hazivumiliki kuona.

Taarifa hizo zimebaini kwamba zaidi ya maiti 40 zimewekwa barabarani katika mji wa Palmyra. Kabla ya kuuawa. Watu wengi walifungwa kamba mikononi kabla ya kuuawa.

Watu waliyo kati ya 200 na 400 ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto waliuawa. Waathiriwa ni pamoja na wafuasi  wa chama cha BAAS na wafuasi wa Bashar Al Assad.

Wapiganaji wenye msimamo mkali walikua wakisachi katika majengo ya serikali, makambi ya jeshi, katika Ofisi ziliyoachwa za Idara ya upelelezi, wakiwatafuta watu waliojificha. Baadhi ya raia waliuawa kwa risasi, na wengine walichinjwa kwa visu.

Wanamgambo wa Islamic State waliingia katika makavazi maarufu ya Palmyra, ambapo waliharibu nakala ya vitu vya kale, kwa mujibu wa mkurugenzi wa mambo ya kale nchini Syria, Maamoun Abdel Karim. Wapiganaji hao wameweka pia walinzi ili kuzuia watu kuingia katika makavazi hayo.

Baada ya vitendo hivyo vichafu viliyotekelezwa na wanamgambo wa Islamic State, ndege za kijeshi za Syria zimeendesha leo Jumatatu, mashambulizi kadhaa ya anga dhidi ya ngome za zamani za wanajeshi wa Syria, ambazo kwa sasa zinadhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.