Pata taarifa kuu
SYRIA-MASHAMBULIZI-MAGONJWA-AFYA

Kitisho cha kuenea kwa magonjwa Syria

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini Syria, vimesababisha watu zaidi ya milioni moja kujeruhiwa.

Mtu huyu alijeruhiwa wakati mji wa Douma nchini Syria uliposhambuliwa, Desemba 21 mwaka 2014.
Mtu huyu alijeruhiwa wakati mji wa Douma nchini Syria uliposhambuliwa, Desemba 21 mwaka 2014. REUTERS/Badra Mamet
Matangazo ya kibiashara

Uhaba wa madawa na vifaa tiba ni moja ya sababu zinazo pelekea kuenea kwa maradhi mablimbali nchini Syria. Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa takwimu ya zaidi ya kesi 6,500 ya homa ya matumbo mwaka huu na kesi 4200 ya surua, ambazo ni miongoni mwa sababu kuu za vifo kwa watoto.

Homa ya matumbo na magonjwa mengine yanaendelea kutokana na ukosefu wa maji safi kwa ajili ya matumizi na kiwango cha chini cha chanjo ambacho kimetoka asilimia 90 kabla ya kuanza kwa mgogoro na kufikia asilimia 52 mwaka huu.

Polio, kifua kikuu, homa ya matumbo surua, au hepatitis, magonjwa yote haya yalikuwa yalitoweka nchini Syria kupitia mfumo madhubuti wa chanjo. Lakini magonjwa haya kwa sasa yamerudi kuwa sugu, na yamekuwa yakipanda kwa kasi.

Kwa mujibu wa Laurent Sury wa Shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka ni matokeo ya moja kwa moja ya hali ya afya ya nchi hiyo.

" Pamoja na kuanguka kwa mfumo wa afya, leo miundombinu ni haba kwa kuendesha kazi vilivyo nchini Syria, hasa kaskazini, ambapo asilimia 46 ya miundombinu iliharibiwa. Hali hii imesababisha kuonekana kwa magonjwa ambayo hayakuweza kuonekana kwa muda mrefu", amesema Laurent Sury

Mikoa yote na makundi yote ya watu yameathirika, watoto ndio wanakabiliwa na mazingira magumu zaidi.

" Kwa upande wa chanjo za mara kwa mara, watoto wenye umri mdogo ndio wamekua wakilengwa, na hivyo kuonekana kuwa ndio waathirika wa kwanza. Chanjo hizo zilikua si tofauti na zile zinazotolewa kwa watu wazima. Watoto hao ni wale walio na umri uliyo chini ya miaka 3 hadi miaka 5", ameongeza Laurent Sury.

Umoja wa Mataifa, kwa upande wake umetangaza kwamba zaidi ya dola bilioni 8 huenda zikahitajika katika mwaka 2015 kwa kutoa msaada kwa watu milioni 18 wanaouhitaji nchini Syria na kanda nzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.