Pata taarifa kuu
UFARANSA-UTURUKI-SYRIA-Usalama

Paris yaunga mkono kuundwa kwa eneo huru kati ya Syria na Uturuki

Rais wa Ufaransa, François Hollande, ameunga mkono pendekezo la Uturuki la kuundwa kwa eneo huru kati ya Syria na Uturuki.

REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Rais Hollande ameongea kwa simu na mwenziye wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, akimueleza kuunga mkono pendekezo hilo. Hata hivo Marekani imesema iko tayari kuzungumzia suala hilo.

Eneo hilo litatumiwa kwa kuwapokea wakimbizi wanaoyakimbia mapigano kaskazini mwa Syria, ambapo wanamgambo wa kikurdi wanapambana na wapiganaji wa Dola la Kiislam.

François Hollande, ameunga mkono pendekezo hilo la Uturuki ili kuepusha mauaji ya halaiki kaskazini mwa Syria, baada ya wapiganaji wa Dola la Kiislam kuendelea kuyateka baadhi ya maeneo ya Kobane.

Rais wa Uturuki alipendekeza mara kadhaa kundwa kwa eneo huru kati ya Syria na Uturuki na kujizui kushambulia kaskazini mwa Syria ili kulinda maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa Syria wenye msimamo wa wastani dhidi ya Bashar Al Assad. Wakimbizi wa syria nchini Uturuki ni takribani 200,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.