Pata taarifa kuu
IRAQ-MAREKANI-Baraza la mawaziri

Iraq: baraza la mawaziri latangazwa, Marekani yapongeza

Waziri wa mambo ya nje wa marekani john Kerry amelikaribisha baraza jipya la mawaziri lililotangazwa jana juma tatu nchini Iraq, na kusema kuwa baraza hilo litaleta mustakabali wa taifa hilo.

Waziri mkuu mpya wa Iraq, Haidar Al Abadi akiwa Bungeni mjini Baghdad, nchini Iraq.
Waziri mkuu mpya wa Iraq, Haidar Al Abadi akiwa Bungeni mjini Baghdad, nchini Iraq. REUTERS/Ahmed Saad
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Haidar al Abadi, amewaambia waandishi wa habari kuwa huenda serikali hiyo ikasababisha nchi yake kuondokana na makundi ya wapiganaji wanaotishia usalama wa taifa hilo, endapo kutakuwa na kuaminiana miongoni mwa wananchi.

Hata hivyo hakuna Waziri wa ulinzi wala wa mambo ya ndani ya nchi aliyetangazwa mpaka sasa. Lakini waziri mkuu wa nchi hiyo amesema atafanya uteuzi wa mawaziri hao kwa muda wa wiki moja.

Akisisitizia msimamo wa Marekani, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amesema kwamba serikali yake itashirikiana kwa karibu na serikali hiyo.

Nafasi nyingine za mawaziri zimejazwa kwa mujibu wa makubaliano kati ya Washia walio wengi, Wasunni hali kadhalika na Wakurd walio wachache.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.