Pata taarifa kuu
SYRIA

Ban alitaka Baraza la Usalama kuiwekea vikwazo vya silaha nchi ya Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vya silaha nchini Syria,kama hatua ya kuitikia kilio cha kukomesha vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon (AFP/Stan Honda)
Matangazo ya kibiashara

Ban ameainisha agenda yenye vipengele sita kutaka kusitishwa haraka kwa vurugu, hali mbaya ya kibinadamu na mwitikio wa dhati na wa pamoja wa kimataifa.

Mgogoro,huo ambao kwa sasa umeua zaidi ya watu 160,000, umelitia ganzi Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa, ambalo limegawanyika kutokana na kutokukubaliana kati ya mataifa ya Magharibi na Urusi ambayo ni mshirika wa Syria.

Akihutubia jamii ya wa Asia jijini New York,jana Ijumaa Ban amesema kuwa ni muhimu kuzuia kuingizwa kwa silaha nchini humo na kuongeza kuwa si uwajibikaji kwa mataifa na mashirika ya kigeni kuendelea toa msaada wa kijeshi kwa makundi yanayofanya mauaji nchini Syria.

Ban pia amesema ikiwa mgawanyiko ndani ya baraza hilo utaendelea kukwamisha hatua hiyo, anaziomba nchi kuchukua uamuzi huo binafsi na kuzitaka nchi jirani na Syria kuweka udhibiti imara katika kutumia mipaka ya nchi zao na anga la nchi hizo kwa kuingiza silaha nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.