Pata taarifa kuu
IRAQ-Usalama

Iraq: watu 19 wauawa katika mashambulizi tofauti mjini Bagdad

Watu kumi wameuawa katika mashambulizi ya mabomu ya liyotegwa ndani ya gari katika mitaa inayokaliwa na waislamu wa madhehebu ya washia mjini Bagdad, nchini Iraq, wakuu wa usalama na vyanzo vya hospitali wamethibitisha.

Iraq inakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara, na kusababisha watu kupoteza maisha.
Iraq inakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara, na kusababisha watu kupoteza maisha. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Milipuko sita imetokea mapema asubuhi na kusababisha watu 44 kujeruhiwa. Maeneo kunakokusanyika watu wengi ndiio ya melengwa na mashambulizi hayo.

Shambulio baya lilitokea katika mtaa wa Jamila, kaskazini mwa Bagdad, na kusababisha vifo vya watu watatu na 11 kujeruiwa.

Mabomu mengine yaliyotgwa ndani ya magari yalilipuka karibu na makao makuu ya polisi katika nji wa Baladiyat, mashariki mwa Bgdad, na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 10 kujeruhiwa. Milipuko mingine imetokea katika mitaa ya Sadr City, Our na Karrada.

Iraq inakabiliwa na mashambulizi ya kawaida na ya kuvizia siku baada ya siku na kusababisha vifo vya watu 25 kwa siku, ambapo inakadiriwa kwamba vifo vinavyotokea mwaka huu ni sawa vile vliyotokea mwaka 2008, wakati taifa hilo lilikua lilitoka katika machafuko mabaya ya kidini, baada ya kuvamiwa na Marekani mwaka 2003.

watu 25 ewanakadiriwa kuuwawa kwa siku nchini Iraq kutokana na mashambulizi ya mabomu.
watu 25 ewanakadiriwa kuuwawa kwa siku nchini Iraq kutokana na mashambulizi ya mabomu. Reuters/Jaafer Abed

Viongozi wa Irak wanabaini kwamba machafuko hayo yanachochewa na machafuko yanayotokea katika nchi jirani, hususan Syria. Lakini wataalam na wanadiplomasia wanathibitisha kwamba machafuko yanayotokea nchini Irak yanasababishwa na na hasira ya waislamu kutoka madhehebu ya Suni, waliyo wadogo ukilinganisha na madhehebu mengine, ambao wanaonekana kutengwa na kunyanyaswa na viongozi wa Iraq.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.