Pata taarifa kuu
UTURUKI

Waziri mkuu nchini Uturiki Recep Tayyip Erdogan ametangaza baraza lake jipya la mawziri wakati wito wa kumtaka ajiuzulu ukiendelea kutolewa

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelifanyia marekebisho baraza lake la Mawaziri siku moja tu baada ya mawaziri watatu kujiuzulu kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi.Waziri mkuu Erdogan amewateua mawaziri wapya kumi kuchukua nafasi ya wale waliachishwa kazi baada ya Mashauriano na rais Abdullah Gul.

REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mawaziri waliojiuzulu ni waziri wa mazingira Erdogan Bayraktar, ambaye baada ya kufanya hivyo alimtaka Waziri Mkuu kujiuzulu pia.

Polisi wanachunguza tuhuma za baadhi ya Mawaziri kuhamisha fedha za serikali nchini Iran, ambazo zilikuwa zimetengewa kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali.

Bayraktar na mawaziri wenzake watatu wamekanusha kuhusika na tuhuma hizo za ufisadi kwa kile wanachosema ni siasa.

Waziri Mkuu Erdogan amewatahumu wapinzani wake kwa kuendeleza siasa kwa lengo la kuisambaratisha serikali yake.

Waandamaji wameendelea kushuhudiwa kartika miji ya Istambul na Ankara nchini humo wakimtaka waziri mkuu kujiuzulu.

Polisi mjini Istanboul imawasambaratisha waandamaji zaidi ya elfu tano baada ya kuzuka ghasia katika kata ya Kadikoy karibu na mto Istanbul

waandamanaji hao walikuwa kauli mbiu za kumkashifu waziri mkuu ambaye anakabiliw ana changamoto kubwa za kisiasa tangu kuchukuw amadaraka ya kuongoza serikali mwaka 2002.

Wito wa kuandamana umetolewa katika miji mbalimbali nchini humo kuhakikisha wanaungusha utawala wa Ankara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.