Pata taarifa kuu
IRAQ

Idadi ya waumini wa Shia waliouawa mjini Baghdad yaongezeka

Idadi ya waumini wa Shia nchini Iraq waliouawa kutokana na mashambulizi ya siku ya jumatatu imefikia takriban watu 67. Taarifa toka nchini humo zinaeleza wanamgambo kumi wameuawa na vikosi vya usalama nchini humo huku Wizara ya Mambo ya ndani ikionya juu ya kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi 11 yalitekelezwa ndani ya magari na kutikisa mji Mkuu Baghdad na kusabisha idadi kubwa ya washia kusini mwa mji huo kuathiriwa huku zaidi ya mia mbili wakipata majeraha.

Zaidi ya watu 800 wameuawa mwezi huu, na zaidi ya 3000 wameuawa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon ameeleza kuwa Iraq inaelekea kwenye hatua mbaya zaidi ya wimbi la machafuko kuwahi kutokea tangu mwaka 2008.

Sekta ya uchumi wa Taifa hilo imeendelea kutetereka kutokana na mashambulizi hayo ya mara kwa mara.

Mzozo wa jamii ya Waumini wa Sunni na Shia ulianza mwaka 2006 na 2007, baada ya maelfu ya watu kuuawa kwa sababu ya imani zao huku wengine wakilazimika kukimbia makazi yao wakihofia kuuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.