Pata taarifa kuu
SYRIA

Rais wa Urusi na Waziri mkuu wa Israel wajadiliana kuhusu mzozo wa Syria

Rais wa Urusi Vladimir Putin na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamejadili mzozo wa Syria leo Jumanne huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu Urusi kupeleka silaha katika serikali ya Damascus na kuongeza idadi ya vifo.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu timesofisrael.com
Matangazo ya kibiashara

Wakati wakianza mazungumzo hayo Putin amemwambia Netanyahu kuwa anashawishika kuzungumza naye kuhusu hali ya mambo katika ukanda huo na hasa nchini Syria ambapo Netanyahu amesema kuwa kwa pamoja wataweza kufanikisha usalama na uimara kwa taifa hilo.

Netanyahu ni kiongozi mwingine wa dunia ambaye amebisha hodi kwa rais Putin kwa ajili ya mazungumzo kuhusu Syria katika siku za karibuni, baada ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kukutana na kiongozi huyo wa Urusi wiki iliyopita.

Katika mwamko huo wa mazungumzo na Netanyahu katika makazi ya likizo ya Putin katika mji wa mapumziko wa kusini wa Sochi, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon anatarajia kusafiri kwenda nchini Urusi baadaye wiki hii.

Mataifa ya Magharibi na Urusi wamekuwa mara kwa mara katika msuguano juu ya migogoro ya Syria, na Marekani na Ulaya zikiituhumu Urusi kwa kutafuta kuunga mkono utawala wa Rais Bashar al-Assad na kuisambazia serikali yake vifaa vya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.