Pata taarifa kuu
Marekani

Rais Obama ahitimisha ziara yake Mashariki ya Kati

Rais wa Marekani Barack Obama amerejea nyumbani baada ya ziara ya siku nne kutafuta kuimarisha ushiriki wake katika amani ya Mashariki ya Kati, ziara iliyoambatana na kuiunga mkono Israel. 

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama REUTERS/Jason Reed
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya rais Obama katika ukanda huo ilitawaliwa na kauli za kuihakikishia Israel kuwa Marekani iko makini katika kukabiliana na vitisho vya Iran na kuhakikisha uwepo wa matumaini ya kupatikana kwa amani baina ya Palestina na Israel.

Rais Obama pia akiwa katika mkutano na mfalme Abdullah wa II ameonya juu ya wasiwasi kuwa huenda Syria ikajitenga kutokana na itikadi kali kama sera yake yenyewe kuelekea katika vita kali ya madhehebu ya kidini na kutishia kuligawa taifa hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.