Pata taarifa kuu
SYRIA

Mwandishi wa habari auawa kwa kupigwa risasi katika mapigano yanayoendelea nchini Syria

Mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Al Jaazera Mohammed Hourani ameuawa jana ijumaa baada ya kupigwa risasi alipokuwa akiripoti kuhusu mapigano yanayoendelea kuitikisa nchi ya Syria.

AFP/YouTube/Al-Jazeera
Matangazo ya kibiashara

Al Jaazera yenye makao makuu nchini Qatar imethibitisha taarifa za kifo hicho na kusema kuwa Hourani alikutwa na umauti baada ya kupigwa risasi na vikosi vinavyomtii Rais wa Syria Bashar al Assad.

Hourani ameuawa siku moja baada ya Mwandishi wa habari mwingine raia wa Ufaransa Yves Debay kuuawa kwa kupigwa risasi kaskazini mwa nchi hiyo katika mji wa Aleppo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa AFP na Shirika la Waandishi wa Habari wasiokuwa na mipaka lenye makao yake makuu jijini Paris Ufaransa, Waandishi wa habari wapatao 20 wameripotiwa kuuawa tangu kuzuka kwa mapigano ya kuung'oa madarakani utawala wa Rais Bashar al Assad mwezi machi mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.