Pata taarifa kuu
ISRAEL

Kampeni za uchaguzi mkuu zazinduliwa rasmi nchini Israel

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amezindua rasmi kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe ishirini na mbili ya mwezi januari mwaka 2013 na kuwataka wapiga kura kumchagua tena kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo huku akiahidi kulipa kipaumbele swala la kupambana na Iran dhidi ya mpango wake wa nyuklia.

REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Akiwahutubia wafuasi wa chama chake cha Likud Netanyahu amewaambia kuwa yeye ndiye anayefaa kuzuia hofu inayotolewa na Iran dhidi ya Israeli, hivyo ni bora wampe kura ya kuendelea na wadhifa huo ili kuwalinda wananchi wake.

Netanyahu amesema mpango wa nyuklia wa Iran lazima usimame, Israeli na mataifa kadhaa ya magharibi wameendelea kuituhumu Iran kwa kutaka kujipatia bomu za nyuklia jambo ambalo limekuwa likikanushwa vikali na serikali ya Iran.

Mbali na hayo Netanyahu amejipongeza kwa kustawisha uchumi wa taifa hilo na kuweka wazi sera zake za baadaye iwapo atachaguliwa tena huku akitetea mpango wake wa amani na majirani zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.