Pata taarifa kuu
Afghanistani

Kamanda wa juu wa Kundi la Taliban auawa sambamba na Wapiganaji wake 24 nchini Afghanistan

Kamanda wa juu wa kundi wa Kundi la Taliban na wapiganaji wake 24 wameuawa katika mapigano na Vikosi vya Usalama vya Afghanistan Mapigano ambayo yamesababisha Polisi watano kuuawa, Maafisa nchini humo wamethibitisha hii leo.

Wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan
Wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan Reuters/Mohammad Shoiab
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinaseme Kundi la Taliban lilishambulia eneo la Soko na kuua Polisi Watano hatua ambayo baadae ilisababisha kutokea kwa Mapambano kati ya Taliban na Vikosi vya Usalama.
 

Wanamgambo hawa wanadhibiti eneo la kusini na Mashariki mwa Afghanistan, lakini Miaka ya hivi Karibuni Wanamgambo wa kiislam wameanza kujipenyeza kwenye maeneo yenye hali ya utulivu kama eneo la Kaskazini mwa Nchi hiyo.
 

Mbali na kuondolewa kutoka Serikalini mwaka 2001, Operesheni iliyoongozwa na Marekani, kundi la Taliban wamekuwa na Serikali yao inayoongozwa na Magavana wanaokuwa na Jukumu la kukusanya Kodi na Serikali yenye utawala wao wa Kisheria.
 

Majeshi ya kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO yana vikosi vyake takriban wanajeshi 100,000 vikisaidia Serikali ya Rais wa Nchi hiyo Hamid Karzai katika kupambana na Wanamgambo,hata hivyo wanatarajiwa kuondoka nchini humo, mwishoni mwa mwaka 2014.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.