Pata taarifa kuu
SYRIA

Koffi Annan aahidi kuzungumza na Upinzani wa Syria juu ya Majadiliano yake na Rais Assad

Msuluhishi wa kimataifa wa Mgogoro wa Syria, Kofi Annan amesema alikubaliana na Rais wa nchi hiyo, Bashar Al Assad juu ya hatua za kumaliza Mgogoro wa Syria .

Mkuu wa Operesheni ya Majeshi ya NATO nchini Syria, Robert Mood (kushoto), akiwa na Msuluhishi wa Mgogoro wa Nchi hiyo, Koffi Annan
Mkuu wa Operesheni ya Majeshi ya NATO nchini Syria, Robert Mood (kushoto), akiwa na Msuluhishi wa Mgogoro wa Nchi hiyo, Koffi Annan Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Annan amesema wamejadiliana juu ya umuhimu wa kumaliza mapigano na namna ya kufikia lengo hilo, na kuongeza kuwa atazungumza na Upinzani juu ya yale aliyojadili na Assad.
 

Kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wa Mataifa, ambao waangalizi wake wako nchini Syria wamekuwa wakikwamishwa kutokana na Machafuko yanayopamba moto na kusisitiza umuhimu wa kuendelea na mazungumzo mapendekezo ambayo yaliridhiwa na Rais Assad.
 

Gazeti la Karibu na Serikali ya Syria, Al Watan limesema Annan na Assad wamezungumza juu ya matokeo ya Mkutano wa Marafiki wa Syria uliofanyika Geneva nchini Uswiss Mwishoni mwa Mwezi jana.
 

Ripoti ya Gazeti hilo imesema katika Mkutano huo walijadili juu ya utekelezwaji wa Matokeo ya Mkutano huo ikiwemo uundwaji wa Serikali ya Mpito nchini Syria kati ya Serikali na wawakilishi wa Upinzani.
 

Mataifa Rafiki ya Syria yalikubaliana juu ya Mpango wa uundwaji wa Serikali ya Mpito makubaliano ambayo hayakumtaka Assad kuondoka Madarakani, ingawa Mataifa ya Magharibi na Upinzani wameeleza kutoona umuhimu wa Assad katika Serikali ya Pamoja.
 

Hatua hiyo imekuja wakati ambapo kumekuwepo na taarifa za kuuawa kwa Watu zaidi ya 17,000 tangu Mwanzoni mwa Mwezi March Mwaka jana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.