Pata taarifa kuu
Syria

Assad ajibu Mapendekezo ya Umoja wa Mataifa ya kukomesha Mauaji nchini Syria

Rais wa Syria Bashar Al Asaad amejibu mapendekezo yaliyopendekezwa kwake na Mjumbe wa Umoja wa MataIfa Koffi Annan juu ya namna ya kumaliza machafuko nchini humo.

Mjumbe wa UN, nchini Syria akizungumza na Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Mjumbe wa UN, nchini Syria akizungumza na Rais wa Syria, Bashar Al Assad Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Koffi Annan Ahmad Faawzi amethibitisha majibu kutoka kwa Rais Asaad na kusema kuwa sasa yanatathiminiwa na baadaye hivi leo,Mjumbe huyo wa amani anatarajiwa kutoa tamko mjini Geneva nchini Uswizi.

Shinikizo kutoka kwa Mataifa ya magharibi,zinaendelea kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuichukulia hatua Serikali ya Asaad ambayo inadaiwa kutekeleza vifo vya maelfu ya watu kwa kipindi cha Mwaka mmoja sasa.

Mashirikja ya kutetea haki za biandamu yanasema majeshi ya serikali yanaendelea kutekeleza mauji kila siku hasa Kaskazini mwa nchi hiyo .

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.