Pata taarifa kuu
Syria

Koffi Annan aondoka Damascus bila kufanikisha lengo la kukomesha mauaji nchini Syria

Mjumbe wa amani wa umoja wa mataifa kuhusu mgogoro unaonedelea nchini Syria Koffi Annan ameondoka Damascus bila kufanikisha kumaliza vitendo vya umwagaji damu, hata hivyo ameshauriana na rais Bashar Al Asaad kuhusu namna ya kumaliza machafuko yanayoendelea nchini humo kwa karibu mwaka mmoja sasa.

Mjumbe wa mzozo wa Syria, Koffi Annan lipokutana na Rais Bashar Al Assad
Mjumbe wa mzozo wa Syria, Koffi Annan lipokutana na Rais Bashar Al Assad Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Licha ya Annan kushauriana na rais Asaad mwishoni mwa juma lililopita mashambulizi majeshi ya srrikali yameendelea kuwashambulia waandamanaji katika mji wa Idlib unaopakana na nchi ya uturuki.
 

Koffi Annan anasema mazungumzo yake ka rais Asaad yalikwenda vizuri na kueleza na amatumaini ya kufanikiwa,licha ya kukiri kuwa haitakuwa rahisi kumaliza mgogoro huo amabo anasema tayari amewasilisha mapendekezo kadhaa ya namna ya kumaliza machafuko nchini humo kwa Rais Assad.
 

Katika hatua nyingine hii leo kundi la upinzani limetoa wito wa kuishwa kwa mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, UN kufuatia Ripoti ya kuuawa kwa wanawake takriban 50 na watoto mjini Homs.
 

Baraza la Taifa la Syria limesema linafanya mawasiliano na Mashirika yote na nchi Rafiki wa watu wa Syria ili kusisitiza kufaniyika mkutano huo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.