Pata taarifa kuu
SYRIA-DAMASCUS

Mkuu wa tume ya misaada ya Umoja wa Mataifa yuko njiani kueleka kwenye mji wa Homs

Mkuu wa tume ya misaada ya umoja wa Mataifa UN, Valerie Amos hatimaye amewasili mjini Damascus Syria ambako amefanya mazungumzo na viongozi wa serikali kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye mji wa Homs ambao umekuwa kwenye mashambulizi kwa majuma mfululizo. 

Valerie Amos mkuu wa tume ya misaada ya Umoja wa Mataifa
Valerie Amos mkuu wa tume ya misaada ya Umoja wa Mataifa UN Photo/Eskinder Debebe
Matangazo ya kibiashara

Kuwasili kwa mkuu huyo wa tume ya misaada kumekuja ikiwa zimepita siku chache toka Serikali ya Syria itangaze kumzuia kiongozi huyo kuingia nchini humo ambapo baadae ilibadili msimamo wake na kumruhusu kufanya ziara nchini humo.

Bi Valerie Amos anatarajiwa kuwasili kwenye mji wa Homs hii leo ambako atafanya ziara kwenye miji midogo iliyoko mjini humo kujionea athari ambazo zimetokana na mapgano kati ya majeshi ya Serikali na jeshi huru la Syria.

Mashirika ya msalaba mwekundu bado yake nje ya mpaka wa mji wa Bab Amr mji ambao nao umeelezwa kuathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa ngome kubwa ya wapiganaji wa jeshi huru.

Ziara ya Amos inakuja wakati ambapo hii leo pia katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan aliyeteuliwa na katibu mkuu wa sasa kuwa msuluhishi mkuu wa mgogoro wa Syria, anatarajiwa kuwasili kwa mazungumzo na pande zinazokinzana.

Kiongozi huyo ataambatana na wajumbe aliowateua kusaidiana na nao kutatua mgogoro wa Syria ambapo pamoja na mambo mengine wanakazi ya kuzishawishi pande hizo kurejea kwenye meza ya mazungumzo kumaliza mauaji dhidi ya raia.

Wakati ujumbe huo ukiwasili hapo jana Serikali ya China ilimtuma balozi wake maalumu Li Huaxin ambaye amefanya mazungumzo na Walid al-Muallem ambaye ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Syria kufahamu kwa undani kinachoendelea nchini humo.

Ujumbe wa China unafuatia kauli ya rais Hu Jintao ambaye amesisitiza njia ya mazungumzo kutumika kumaliza mzozo ulioko nchini humo badala ya kutumika kwa nguvu za kijeshi.

Rais Bashar al-Asad ameendelea kuyashutumu mataifa ya magharibi kwa kuchochea chuki miongoni mwa wananchi hali ambayo ameeleza kuwa inachangia kuendelea kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Zaidi ya watu elfu mbili wanaelezwa kuyakimbia makazi yao kutokana na machafuko yanayoendelea kwenye mji wa Homs.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.