Pata taarifa kuu
IRAQ-SYRIA

Iraq yaitaka Syria kushiriki kilele cha mkutano wa mataifa ya kiarabu

Serikali ya Iraq kupitia waziri mkuu wake Nur Al Malik imetaka Syria kushiriki katika kilele cha mkutano wa mataifa ya kiarabu ambao unataraji kufanyika Baghdad mwishoni mwa march.

Makundi mbalimbali yamekuwa yakipambana na vikosi vya serikali ya Syria kupinga utawala huo.
Makundi mbalimbali yamekuwa yakipambana na vikosi vya serikali ya Syria kupinga utawala huo. REUTERS/Ali Hashisho
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu Nur Al Malik alisema hayo akiwa katika mahojiano na kituo kimoja cha televishen nchini iraq na kuongeza kuwa anamatumaini kuwa viongozi wote wa mataifa ya kiarabu watashiriki mkutano huo utakao fanyika mwishoni mwa mwezi march mwaka huu.

Nchi wanachama wa kiarabu walipiga kura mnamo mwezi Novemba mwaka jana ili kuiondoa ushiriki wa Syria katika umoja wa kiarabu kutokana na ghasia za nchini humo.

Raisi wa Syria Bashar Al Assad amekuwa akifanya ukandamizaji kwa waandamanaji na kukithiri umwagaji damu kwa raia wake ambapo zaidi ya watu elfu sita wamepoteza maisha tangu machi 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.