Pata taarifa kuu
Syria

Zaidi ya watu 80 wapoteza Maisha mjini Homs nchini Syria

Zaidi ya watu 80 wameuawa nchini Syria jana, wengi wao wakiwa mji uliokumbwa na Machafuko, Homs, shambulio ambalo Rais wa Marekani, Barak Obama amesema ni vitendo vya umwagaji damu vilivyokithiri.

Rais wa Syria Bashaar Al Assad
Rais wa Syria Bashaar Al Assad
Matangazo ya kibiashara

Shirika la waangalizi wa haki za Binaadam lenye Makazi yake nchini Uingereza, limesema kuwa takriban watu 83 waliuawa nchini humo jana, wakati vikosi vilipokuwa vikipambana na wapinzani wa Rais wa nchi hiyo, Bashar Al Assad.
 

Nao wanaharakati nchini Syria wamesema kuwa watu takriban 400 wameuawa ndani ya siku sita mjini Homs.
 

Waziri mkuu wa Uingereza,David Cameron amesema utawala wa Assad hivi sasa umekuwa wa kujeruhi na kuuwa Raia wake wenyewe.
 

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu ameitaka jumuia ya kimataifa kuutatua mzozo wa Syria ulioshika kasi baada ya waandamanaji kudai Assad kuondoka Madarakani.
 

Nae mkuu wa jumuia ya nchi za kiarabu amemuaomba kiongozi wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kuumini ujumbe wa Mawaziri wa mambo ya nje wa umoja huo wakati huu wanapoelekea kukutana mwishoni mwa juma hili, ili kuunga Mkono jitihada za Jumuia ya Kimataifa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.