Pata taarifa kuu
Syria

Rais wa Syria, Bashar Al Assad asema ana nia ya kumaliza machafuko nchini mwake

Urusi imeweka bayana kuwa Rais wa Syria Bashar Al Assad yupo tayari kumaliza umwagaji wa damu ambao umekuwa ukishuhudiwa katika nchini yake wakati huu Utawala wake ukilaumiwa kupiga mabomu Jiji la Homs.

Rais wa Syria Bashaar Al Assad
Rais wa Syria Bashaar Al Assad
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imekuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergie Lavrov kukutana na Rais wa Syria Bashar Al Assad na kujadili kwa kina kile ambacho kinaendelea kushuhudiwa katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko.

Rais Assad amemhakikishia Waziri huyo kuwa yupo tayari kumaliza machafuko ambayo yameziid kuchacha na kuchangia umwagaji wa damu mkubwa katika nchi hiyo kutokana na wapinzani kutaka mabadiliko ya kisiasa.

Rais Assad amesema kitu cha msingi ni kuhakikisha maisha ya wananchi wa Syria wanakuwa kwenye usalama lakini wataendelea kukabiliana na magadidi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuleta machafuko.

Nae Lavrov aliyerejea kutoka kwenye mazungumzo na Assad amesema kuwaondoa wanadiplomasia mjini Damascus si njia muafaka ya kufikia malengo ya utekelezaji wa mpango wa jumuia ya nchi za kiarabu.

Katika hatua nyingine Wanaharakati wamezidi kuishutumu serikali ya Syria kutokana na kuendelea na mashambulizi yao katika Jiji la Homs wakiamini wananchi wengi wamepoteza maisha kwenye mashambulizi hayo ya mabomu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.