Pata taarifa kuu
Syria

Takriban Watu 100 wauawa nchini Syria baada ya Vikosi vya Serikali ya nchi hiyo kushambulia Raia

Takriban watu 100 wameuawa nchini Syria siku ya jumatau katika mapigano,baada ya vikosi vya serikali ya nchi hiyo kushambulia raia mjini Homs na maeneo mengine.

Rais wa Syria Bashaar Al Assad
Rais wa Syria Bashaar Al Assad
Matangazo ya kibiashara

Waangalizi wa maswala ya haki za Binaadam wamesema watu 69 wameuawa mjini Homs na vijiji vya karibu yake huku wengine 13 wakiuawa kaskazinimagharibi mjini Idlib.
 

Shirika hilo limedai kuwa watu 16 wameuawa katika mapigano katika miji mingine ikiwemo Aleppo, kuelekea Kaskazini na wengine 15 karibu na mji mkuu, Damascus.
 

Takwimu hizi za vifo zinakuja wakati huu ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergie Lavrov amezuru Damascus na kukutana na viongozi wa serikali na kujadili namna ya kuhakikisha umwagaji wa damu unamalizwa.

Uingereza ni moja ya nchi ambayo imekuwa ikihaha kuhakikisha inamaliza mauaji ambayo yanashuhudiwa nchini Syria kwa sasa na hapa Waziri wake wa Mambo ya Nje William Hague anaeleza hatua wanazochukua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.