Pata taarifa kuu
Palestina-Israel

Israel na Palestina wafanya mazungumzo ikiwa miezi kumi na mitano

Wapatanishi wa Israeli na Palestina wamefanya mazungumzo ikiwa ni miezi kumi na mitano tangu kuvunjika kwa mazungumzo ya mara ya mwisho na kuahidi kukutana tena ijumaa hii.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas REUTERS/Mohamad Torokman
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo uliofanyika nchini Jordan yamelenga kufufua mazungumzo ya awali yaliyogonga mwamba kuhusu ujenzi wa makazi ya kudumu kwenye ukanda wa Gaza.
 

Waziri wa maambo ya nje wa Jordan Nasser Judeh amesema kuwa mazungumzo ya hapo jana yameonesha muelekeo chanya na ana imani kuwa viongozi wa nchi hizo mbaili watapata suluhu ya mgogoro walionao.
 

Judeh, aliyehodhi mkutano huo mjini Amman nchini Jordan, ametoa angalizo la kufanyiwa kazi maendeleo na maazimio ya mkutano huo ili kutopoteza maana ya mazungumzo hayo.
 

Mkuu wa sera za kigeni ndani ya umoja wa Ulaya Catherine Ashton ameitaka Israel na Palestina kuendelea na jitihada za kutafuta amani kati ya mataifa hayo mawili.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.