Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA

Israel na Palestina kufanya mazungumzo kesho

Viongozi wa Palestina na israel wanaohusika katika mazungumzo ya kusaka amani ya kudumu kwenye eneo la ukanda wa gaza, kwa mara ya kwanza wanatarajiwa kukutana mjini Jordan kesho kwa mazungumzo. 

REUTERS/Mohamad Torokman
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unaitishwa ikiwa umepita mwaka mmoja toka kuvunjika kwa mazingumzo kati ya wawakilishi wa nchi hizo yaliyogonga mwamba kufuatia israel kuendelea na ujenzi wa makazi kwenye eneo hilo.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na mshauri mkuu wa palestina kuhusu mgogoro huo Saeb Erakat na mwakilishi wa waziri mkuu wa Israel Yizak Mocho ambapo pamoja nao ujumbe toka nchi za marekani, Urusi na Umoja wa ulaya wanatarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo.

Hata hivyo msemaji wa chama cah Palestina Liberation Organization PLO Xavier Abu Eid amesema kuwa mkutano huo sio wa kuanza mazungumzo rasmi bali ni wa kutengenza mazingira mazuri ya mazungumzo rasmi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.