Pata taarifa kuu
IRAQ

Zaidi ya watu 57 wauawa na wengine 154 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu nchini Iraq

Watu zaidi ya Ishirini na tatu wameripotiwa kuuawa katika matukio kumi na tatu tofauti nchini Iraq kwenye miji tofauti kufuatia mfululizo wa milipuko ya kutegwa na watu wasiofahamika.

Moshi ukionekana kutanda katika eneo la mji wa Baghdad baada ya mashambulizi ya mabomu nchini Iraq.
Moshi ukionekana kutanda katika eneo la mji wa Baghdad baada ya mashambulizi ya mabomu nchini Iraq. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchini Iraq imesema kuwa kumetokea mashambulizi ya mabomu ya kutegwa kwenye maeneo kumi na tatu tofauti ikiwemo mjini wa Baghadad, al-Amil uliopo kusini mwa nchi hiyo, Halawi pamoja na Karrada mji ulioko jirani na Badhadad.

Mashambulizi hayo yanatokea wakati ambapo kumeendelea kuzuka hofu ya machafuko ya kisiasa kufuatia mahakama kuu mjini Baghadad kutoa hati ya kukamatwa kwa makamu wa rais wa nchi hiyo Tariq al-Hashimi kwa tuhuma za ugaidi.

hali hiyo imeendelea kuzua hofu ya kuendelea kufanywa mashambulizi na makundi ya kigaidi yaliyoko nchini humo wakitumia mwaya huu ambapo vikosi vya majeshi ya Marekani vimeanza kuondoka nchini Iraq.

Hapo jana waziri mkuu wa nchi hiyo Nouri al-Malik alitoa wito kwa serikali ya Kikkurdi kumkabidhi kwa vyombo vya dola makamu huyo wa rais ambaye ameendelea kuomba hifadhi kwa serikali hiyo na kuendelea kukanusha kuhusika na makundi ya Kigaidi.

Wakati huo huo wabunge wa kisuni wameendelea kususia vikao vya bunge la nchi hiyo wakipinga kile ambacho mahakama imeamua wakisisitiza kuwa watafanya hivyo mpaka pale uamuzi huo utakapobatilishwa.

Waziri mkuu Nouri al-Malik ametishia kuwafukuza kazi wabunge hao endapo wataendelea na mgomo wao na kuendelea kuzuka hofu ya kutokea machafuko ya kikoo nchini Iraq.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote ambalo limekiri kuhusika katika mashambulizi ya hii leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.