Pata taarifa kuu
IRAN

Cameron aionya Iran juu ya uvamizi dhidi ya ofisi zake za ubalozi

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon ameionya nchi ya Iran kuhusu hatua ambazo nchi yake itazichukua kufuatia ubalozi wake mjini Tehran kuvamiwa na kundi la wanafunzi.

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron REUTERS/Oli Scarff/POOL
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu cameroon amesema kuwa amesikitishwa na polisi nchini humo kushindwa kuwadhibiti wanafunzi hao walioingia hadi ndani ya uwigo wa ubalozi huo na kushusha bendera yao na kuweka ya Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Heague ameushtumu utawala wa Iran na kutaka nchi hiyo kuulinda ubalozi wake kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kidiplomasia.

Nalo baraza la usalama la umoja wa Mataifa imeitaka mamlaka ya iran kulinda Mali na wafanyakazi wa kidiplomasia na kuheshimu wajibu wake katika kutekeleza hilo.

Siku ya jumapili bunge la Iran lilipiga kura na kulaani uamuzi uliochukuliwa na Uingereza wa kuiwekea vikwazo nchi hiyo na kutishia kuvunja uhusiano na nchi hiyo kama ilivyofanya kwa Marekani miaka 30 iliyopita.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.