Pata taarifa kuu
Syria

Mauaji dhidi ya waandamanaji yaendelea Syria

Mauaji dhidi ya waandamanaji, yanazidi kushuhudiwa nchini Syria na mwishoni mwa juma, waandamanaji wasiopungua 24 waliuawa kwa kupigwa risasi nchini humo, huku kiongozi wa nchi za kiarabu akitazamiwa kuzuru nchini humo.

REUTERS/Handout
Matangazo ya kibiashara

Mauaji nchini Syria yanaendelea kwa mwezi wa tano sasa, huku waandamanaji wakiwa bado wanashinikiza kujiuzulu kwa rais, Bashar Al-Asadd ambaye hadi sasa hajaonyesha dalili za kuondoka mamlakani.
Kiongozi wa Muungano wa Nchi za Kiarabu Nabil Al-Arabi akiwa nchini humo anatarajiwa kukutana na viongozi wa Serikali ya Syria, kutafuta namna ya kumaliza mgogoro huo.
Jamii ya kimataifa, imeishutumu mauaji yanayoendelea nchini Syria na Umoja wa Matifa unakadiria kuwa zaidi ya waandamanaji elfu mbili hadi sasa wamepoteza maisha yao nchini humo.
Umoja wa Ulaya, umemataka Rais Asaad kujiuzulu na tayari umemwekea vikwazo ya kutosafiri yeye pamoja na maafisa kadhaa wa serikali yake huku, Marekani ikisitisha biashara ya mafuta na Syria.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.