Pata taarifa kuu
Syria

Rais wa Iran Ahmadinejad ataka Rais wa Syria azungumze na wapinzani

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad mshirika wa karibu wa rais wa Syria, Bashar Al Assad ametaka kufanyika mazungumzo kati ya Serikali na upinzani kumaliza machafuko yaliyodumu kwa miezi kadhaa nchini humo.

FARS
Matangazo ya kibiashara

Ahmadinejad amesema watu wa Syria lazima waungane kufikia maelewano bila kupoteza maisha ya watu wengine.
Maafisa nchini Iran mara kwa mara wamekuwa wakimtaka Assad kufanya mabadiliko ili kuepuka kupinduliwa kama ilivyofanyika katika mataifa mengine ya Kiarabu.
Hata hivyo Rais Assad ameendelea na msimamo wake wa kutokutaka kuondoka madarakani na amesema hatishwi na nguvu yeyote kutoka nje.
Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikitoa wito wa kumshinikiza Assad kuachia madaraka na kusitisha mashambulizi dhidi ya raia wanaoandamana kupinga utawala wake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.