Pata taarifa kuu
Syria

Mataifa ya Magharibi yataka UN ichukue hatua dhidi ya Syria

Mataifa ya Magharibi yametaka Umoja wa Mataifa, UN kuchukua hatua dhidi ya serikali ya Rais wa Syria Bashar Al Assad ambaye amekaidi agizo la kusitisha mauaji na kuendelea kushambulia wananchi.

RFI
Matangazo ya kibiashara

 

 

Tamko hilo linakuja wakati huu ambapo Marekani ikitangaza vikwazo zaidi dhidi ya Utawala wa Rais Assad huku Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Oscar Fernandez Taranco akisema wajumbe wanataka hatua dhidi ya Syria.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, UN Susan Rice ambaye alipata nafasi ya kuhutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ameendelea kusisitiza Rais Assad amepoteza uhalali wa kuongoza.

Kufuatia kutoka kwa kauli hiyo ndiyo Balozi wa Syria kwenye Umojwa Mataifa, UN Bashar Jaafari aliwataka wale wanaoeneza propaganda za utawala wao kupoteza uhalali kuacha mara moja.

Wakati hayo yakiendelea huko UN taarifa kutoka Syria zinaeleza kuwa watu 17 wamepigwa risasi kwenye Mji wa Homs ukiwa ni muendelezo wa kile ambacho serikali inasema kupambana na ugaidi.

Hali inayoendelea Syria bado ni kitendawili kwa kuwa pamoja na shinikizo linalotolewa na jumuiya ya kimataifa, rais wa nchi hiyo ameshikilia msimamo wake wa kuendelea na mashambulizi dhidi ya raia na kuendelea kutawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.