Pata taarifa kuu
SYRIA

Watu 11 wauawa nchini Syria katika mji wa Kanaker

Wanaharakati nchini Syria wametoa taarifa kuvishutumu vikosi vya serikali kwa kuhusika na mauaji ya wananchi kumi na mmoja katika mji wa Kanaker ulio jirani na mji mkuu Damascus.

Moja ya mabango ya waandamanaji nchini Syria likisomeka "Wote tunataka uondoke, tunataka uhuru wa Demokrasia
Moja ya mabango ya waandamanaji nchini Syria likisomeka "Wote tunataka uondoke, tunataka uhuru wa Demokrasia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ammar Qurabi msemaji wa shirika la kutetea haki za binadamu nchini humo amesema kuwa wanajeshi waliingia katika huo hii leo na kuanza operesheni ya nyumba hadi nyumba kuwasaka wanaharakati ambao wanachochea maandamano nchini humo na kuua watu kumi na mmoja.

Msako huo unakuja kufuatia maandamano yaliyofanyika katika mji huo kushinikiza kujiuzulu kwa serikali ya rais Bashar al-Assad ambaye hata hivyo amesisitiza kutong'atuka madarakani na kuahidi kuwakamata wanaohusika na kuchochea vurugu nchini humo.

Vikosi vya nchini Syria vimeanzisha operesheni ya nyumba hadi nyumba katika miji ya nchini humo wakati huu ambapo wananchi wa taifa hilo wanajiandaa kuingia katika mfungo wa mwezi Ramdhani.

Wanaharakati nchini humo wamekosoa mashambulizi ya askari wa serikali dhidi ya raia wakati ambapo wamesema wananchi wanajiandaa na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mashambulizi hayo yanafanyika licha ya siku ya Jumatatu nchi hiyo kupitisha sheria mpya inayoruhusu kuundwa kwa vyama vipya vya kisiasa na kumaliza miongoz kadhaa ya uatwala wa chama kimoja cha Baath.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.