Pata taarifa kuu
KANDAHAR-AFGHANISTAN

Meya wa Jimbo la Kandahar nchini Afghanistan auawa katika shambulio la bomu

Mtu mmoja asiyefahamika amejitoa muhanga katika jimbo la Kandahar kusini mwa nchi ya Afghanistan na kumuua meya wa jimbo hilo Ghulam Haidar Hameedi, polisi nchini humo wamedhibitisha.

Wanajeshi wa Afganistan wakilinda usalama katika Jimbo la Kandahar
Wanajeshi wa Afganistan wakilinda usalama katika Jimbo la Kandahar REUTERS/Ahmad Nadeem
Matangazo ya kibiashara

Zalmay Ayoubi ambaye ni msemaji wa gavana wa jimbo hilo amedhibitisha kutokea kwa shambulio hilo la bomu lililotekelezwa na mtu asiyefahamika kwenye eneo ambalo Meya huyo alikuwa akihutubia wananchi wa eneo lake.

Akiongelea tukio hilo mkuu wa Polisi wa jimbo la Kandahar Abdul Razaq amesema wakati shambulio hilo likitekelezwa Meya Hameedi alikuwa akifanya mkutano na wazee wa jimbo hilo kuhusiana na mgogoro wa ardhi ambao umeibuka hivi karibuni baada ya Meya huyo kutangaza kuvunjwa kwa baadhi ya nyumba zilizojengwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambulio hilo ingawa polisi wamesema kuwa huenda ni mfululizo wa mashambulizi ya wapiganaji wa Taliban.

Shambulio hilo linakuja ikiwa zimepita wiki mbili tangu kuuawa kwa mdogo wa rais wa nchi hiyo Harmid Karzai, Ahmad Wali katika shambulio la kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake kabla ya wakati wa mazishi ya kiongozi huyo wanamgambo hao kushambulia kwa bomu na kumuua kiongozi mmoja wa kidini katika jimbo hilo.

Kufuatia mashambulizi hayo, hofu imeendelea kutanda nchini humo kuhusu uimara wa vikosi vya serikali kuweza kukabilina na wapiganaji wa Taliban mara baada ya majeshi ya Marekani na washirika wake kuondoka nchini humo.

Tayari rais Harmid Karzai ameanza kufanya mazungumzo na serikali ya Marekani kuangalia uwezekano wa kuviongezea muda vikosi vya nchi yake vilivyoko nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.