Pata taarifa kuu
SYRIA

Maandamano zaidi yaripotiwa nchini Syria huku baadhi ya Magavana wakiachishwa kazi

Rais wa Syria, Bashar Al-Assad ametangaza kumfukuza kazi gavana wa jimbo la Deir az-Zor, Samir Hussein Arnos ikiwa ni baada ya kushuhudia maandamano makubwa ya siku mbili mfululizo katika jimbo lake.

Waandamanaji nchini Syria
Waandamanaji nchini Syria Reuters
Matangazo ya kibiashara

Jumapili jioni rais Assad alimtangaza Samir Othman al-Sheikh mmoja wa maofisa wa kitengo cha usalama wa Taifa kwenda kuziba pengo la Arnos ambaye ameachishwa kazi kwa kushindwa kuzuia maandamano ya siku mbili yaliyofanyika katika jimbo lake.

Hata hivyo pamoja na kumwachisha kazi kama gavana wa Jimbo la Dier, rais Assad amemteua Arnos kwenda kuwa gavana katika jimbo dogo la Qunaitera lililoko jirani na mji wa Damascus mpakani na mji wa Golan Heights.

Zaidi ya wananchi nusu milioni walishiriki katika maandamano ya siku ya Ijumaa yakiwa ni maandamano makubwa zaidi kufanyika katika juma lililopita wakishinikiza kujiuzulu kwa serikali ya rais Assad.

Polisi nchini humo wameendelea na msako wa wanaharakati ambao wanahamasisha maandamano nchini humo, ambapo imewakamata watu kadhaa katika mji wa Damascus na Homs ambako kulifanyika maandamano juma moja lililopita.

Licha ya serikali kutangaza kuanza mazungumzo ya kitaifa na viongozi wa upinzani bado kumeendelea kufanyika maandamano nchini humo baadhi yao wakipinga mazungumzo ya kitaifa na kumtaka rais Assad na serikali yake kujiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.