Kila mwaka dunia hutumia siku 16 kuadhimisha mapambano ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto .
Umoja wa mataifa huongoza kampeni hii na hufanyika kuanzia tarehe 25 Novemba na kumalizika tarehe 10 Desemba ya kila mwaka kwa ajili ya kupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.
Siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991 na tangu wakati huo zaidi ya asasi 6,000 kwa zaidi ya nchi 187 hushiriki katika maadhimisho haya.
Nchini Kenya katika eneo la Kibra baadhi ya kinadada wamethibitisha kuwa visa vya dhulma bado vipo na kati ya wanawake 5 wawili wamedhulumiwa kisaikologia na hata kingono .
Ili kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.