Pata taarifa kuu
Gurudumu la Uchumi

Madeni yanavyoendelea kuzikwamisha nchi masikini kupiga hatua

Imechapishwa:

Athari wa Uviko19 na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, zimesababisha mataifa mengi ya Afrika kushindwa kulipa madeni yake kwa wakati, ambapo hadi kufikia sasa nchi zenye kipato cha chini karibu 22 tayari zinashindwa kulipa madeni yake au zinaelekea kushindwa.

Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika uliofanyika nchini Ethiopia kujadili masula ibuka katika bara hilo
Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika uliofanyika nchini Ethiopia kujadili masula ibuka katika bara hilo AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa IMF na benki ya dunia, Afrika inadaiwa karibu dola za Marekani bilioni 726 na wakopeshaji wa nje, huku sekta binafsi kutoka China ikiwa sehemu ya wakopeshaji wakubwa kwasasa barani Afrika.

Hali hii imezifanya nchi nyingi, kuomba kusamehewa baadhi ya madeni au kufanyika upya kwa utaratibu wa ulipaji.

Lakin je Madeni haya ni kwakiasi gani yataendelea kuzikwamisha nchi masikini kupiga hatua?

Hili ndilo tunalokwenda kulitazama hivi leo kwenye Makala ya Gurudumu la uchumi na  Emmanuel Makundi.

Kujadili hili kwenye line ya simu tutakuwa na Johnson Denge, mchambuzi na mtaalamu wa uchumi akiwa Kenya, lakini kabla ya kumsikia, tusikie kile katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alikisema wakati wa viongozi wa umoja wa Afrika juma lililopita.

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.