Makala kuhusu Tamasha la MOCA lililofanyika huko Kigali Rwanda
Imechapishwa:
Cheza - 19:50
Karibu kuwa nami Jumapili hii katika Makala Changu Chako Chako Changu, makala maalum kuhusu Tamasha lijulikanalo kama MOCA, Movement Of Creative Africas, yaani jukwaa la Viwanda vya Utamaduni na Ubunifu vya Kiafrika (ICC) na diaspora. Jumapili hii siko pekeangu nitakuwa naye mtangazaji mwenzangu ambae tumeambatana pamoja mpaka Kigali nchini Rwanda Florence Kihuwa.
Tamasha la 7 linafanyika kuanzia Juni 30 hadi Julai 3, 2022 mjini Kigali, nchini Rwanda, kwa ushirikiano na Wizara ya Utamaduni, na jiji la Kigal…, toleo ambalo halijawahi kushuhudiwa kuhusu mada “Ubunifu na Sanaa kwa ajili ya mabadiliko!”.
Fursa ya kuelewa jinsi ubunifu na sanaa inavyochangia katika maendeleo ya Afrika.
Mengi zaidi kuhusu MOCA FESTIVAL nimezungumza na Muasisi wa Tamasha hilo Alain Bijek raia wa Cameroon.